TANZANIA BUREAU OF STANDARDS(TBS)
e-Services

Dira

"Matumizi endelevu ya viwango kwa jamii yenye maisha bora".

 

Dhamira

"Kukuza viwango, usalama na uhakiki wa ubora katika viwanda na biashara kupitia uandaaji wa viwango, uhakiki wa ubora, usajili, ukaguzi, upimaji na huduma za ugezi kwa maendeleo endelevu ya kijamii na uchumi".

 

Misingi Mikuu

 

Uadilifu

Tunahakikisha utoaji endelevu wa huduma kwa uaminifu wa hali ya juu na bila upendeleo kwa kuzingatia kanuni za maadili.

Huduma kwa Wateja

Tunatanguliza mahitaji ya wateja kwanza na tuna dhamira ya dhati ya kukidhi matarajio yao kwa wakati na kwa umakini.

Ushirikiano

Tunafanya kazi pamoja kwa kubadilishana uzoefu huku tukiheshimiana ili kufikia malengo ya taasisi.

Uwajibikaji

Tutawajibika kwa matendo yetu, uamuzi wetu na matokeo yake katika kutekeleza majukumu yetu.

Uwazi

Tunahakikisha mawasiliano ya wazi na kutoa mrejesho kwa wadau wetu kwa usawa.

 

Sera ya Ubora

“Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limedhamiria, kwa kuzingatia dhamana iliyopewa, kutoa bidhaa na huduma bora katika utayarishaji wa viwango, usimamizi wa usalama, uhakiki wa ubora na huduma za metrolojia. TBS inahakikisha inakidhi matakwa ya kisheria, mahitaji na matarajio ya wateja, na hata kuyazidi ili kudumisha uaminifu kwao.

TBS hutoa rasilimali na kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji wake ili kuhakikisha kwamba wakati wote wafanyakazi wake wana uwezo wa kutoa bidhaa na huduma bora ambazo ni endelevu.”

 



Settings