Announcements

Posted On: Jan 22, 2025


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ATHARI ZINAZOHUSISHWA NA MATUMIZI YA MAFUTA YA KUPIKIA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilipokea taarifa kuhusiana na uwepo wa madhara ya kiafya yanayohusishwa na matumizi ya mafuta ya kupikia. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa baadhi ya wananchi kutoka mtaa wa Dovya kata ya Makangarawe wamepata athari za kiafya zikiwemo kuumwa tumbo, kuharisha, kuvimba uso, macho kuwasha na kuwa mekundu, kutokwa vipele na ngozi kubabuka baada ya kutumia chakula kilichoandaliwa kwa kutumia mafuta hayo.

Kwa maelezo zaidi tafadhali fungua kiambatanisho kifuatacho;

taarifa kwa umma kuhusu athari zinazohusishwa na matumizi ya mafuta ya kupikia