Maabara
Maabara za TBS zilianzishwa mwaka 1982 kwa lengo la:
(a)Kuwasaidia watengenezaji bidhaa kuongeza au kuimarisha ubora wa bidhaa zao
(b) Kutoka nyenzo za kupimia bidhaa kuhakikisha kufaa kwao kwa matumizi yaliyokusudiwa na;
(c) Kuhakikisha ubora wa bidhaa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi au kuingizwa nchini.
Maabara hizi pia zinatoa nyenzo za kupimia za haraka, sahihi na za siri kwa upimaji wa aina, upimaji wa uhakiki, ushauri wa kiufundi na maelekezo kuhusu mbinu za upimaji na mafunzo ya watumishi wa maabara.
1.Maabara ya Kemia
Maabara ya Kemia inatoa huduma zifufatazo:
a.Upimaji wa kemikali, bidhaa shirikishi na sampuli za mazingira;
b.Mafunzo katika upimaji wa bidhaa yanayohusiana na kemikali na mifumo ya usimamizi wa ubora ya maabara.
c.Kazi ya utafiti wa mazingira kwa ushirikiano
d.Ushauri kwa wenye viwanda.
e.Uratibu wa Mpango wa Kupima ustadi wa Tanzania (TPTS)
f.Kufanya upimaji wa Ustadi wa chumvi ya kula ngazi ya kitaifa na EAC;
g.Kufanya Mpango wa kupima Ustadi wa maji ya kunywa, ngazi ya kitaifa
h.Uratibu wa mpango wa kupima ustadi SADC; na
i.Ufuatiliaji wa ubora wa hewa
2.Maabara ya Kemia ya Chakula
Maabara hii hupima ubora wa vyakula na bidhaa za kilimo. Maabara hii inapima kiasi cha kemikali, asidi, vitamini, unyevu, mafuta na maada nyingine kwenye bidhaa huweza kutambuliwa kupitia maabara hii.
3.Maabara ya Mikrobiolojia
Maabara hii hupima kiasi cha vijiumbe kinachopatikana katika bidhaa mbalimbali.
4.Maabara ya Nguo na Ngozi
Maabara ya Nguo na Ngozi inatoa huduma zifuatazo;
a.Hutoa nyenzo za upimaji kwa tasnia za nguo na ngozi;
b.Kuwapa mafunzo wachambuzi wa nguo, ngozi kuhusu mbinu bora za maabara; na
f.Hukusanya na kusambaza taarifa za kiufundi.
5.Kituo cha Teknolojia ya Ufungashaji
Serikali ya Tanzania iilianzisha kituo cha Teknolojia ya Ufungashaji (PTC) katika Shirika la Viwango Tanzania katika juhudi za kusaidia uendelezaji wa pamoja wa tasnia ya ufungashaji kwa kuimarisha uwezo wa uwekaji viwango na upimaji kwenye eneo la ufungashaji.
Huduma ya ufungashaji zinazotolewa na Kituo cha Teknolojia ya ufungashaji ni Pamoja na;
a.Kupima vifungashio na nyenzo za kufungashia kuhakikisha ubora;
b.Kutoa mafunzo kwa viwanda na wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati (SME) kwa mambo yanayohusu miundo bora ya vifungashio;
c.Kuendesha utafiti na ushauri kwa masuala yanayohusu ufungashaji bora;
d.Kutoa hati kwa wazalishaji bidhaa wengine kwa nyenzo za ufungashaji na vifungashio vilivyotengenezwa kwa mujibu wa viwango vinavyokubalika.
e.Kutoa huduma za upimaji kwa vifungashio na vyenzo za kufungashia
f.Uwezeshaji wa uagizaji na usafirishaji nje ya nchi nyenzo za kufungashia kulingana na viwango vinavyohusika; na
g.Kutoa taarifa kuhusu viwango vya ufungashaji, masharti na teknolojia;
6.Maabara ya Uhandisi Ujenzi
a.Imesanifiwa kwa ajili ya kupima vifaa vya ujenzi pamoja na vijenzi kuangalia sifa kama vile za uwezo/nguvu, ugeuzaji, uimara, mabadiliko ya sehemu na ukubwa; na
b.Hufaya utafiti wa ugani kwa ajili ya vipimo vya uzito na utoboaji wa maeneo ya zege kwenye ujenzi uliyokamilika kwa ajili ya kupima uwezo/nguvu.
7.Maabara ya Uhandisi Mitambo
a.Maabara hii ina vifaa kwa ajili ya kupima vitu vya kimetali kwa kufanya vipimo vya aina mbalimbali kubaini sifa au tabia mbalimbali za metali; na
b.Inatoa huduma za ushauri na uelekezi kama vile kufaa kwa matumizi ya bidhaa inayohitaji vipimo vya jumla vya kimakanika kwa kutumia viwango yva mahali kitaifa na kimataifa
8.Maabara ya Uhandisi Umeme
a.Imesanifiwa kwa ajili ya kupima vyombo vya nyumbani na vifaa vingine vya umeme vya aina hiyo Pamoja na nyenzo za umeme na vifurasi; na
b.Ina vifaa vya kisasa za kudhibiti aina mbalimbali za ukatikaji wa mzunguko wa umeme na kuvuja kwa waya wa kuaridhisha saketi ya umeme kwa ajili ya kupima hali ya uvujaji waya wa kuaridhisha kwenye kikata umeme katika majengo.