Announcements
Posted On: Feb 13, 2026
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU PICHA MJONGEO (VIDEO) ZINAZOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BIDHAA ZA VILAINISHI (ENGINE OIL
Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa za picha mjongeo (video) zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha baadhi ya watu wasio waaminifu wakifungasha bidhaa za vilainishi vya injini (engine oil) katika maeneo yasiyo rasmi, huku wakitumia chapa (brand) za baadhi ya kampuni kinyume na taratibu. Aidha, picha mjongeo nyingine inaonesha namna ya kufuta na kubadili tarehe ya muda wa matumizi wa bidhaa (shelf life) kwenye kifungashio cha aina ya kopo.