Announcements

Posted On: Jul 26, 2022


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI YA MCHANGANYIKO WA SUKARI NA VIKOLEZA UTAMU (ARTIFICIAL SWEETENERS) KWENYE VINYWAJI LAINI VYENYE KABONI (CARDONATED SOFT DRINK)

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepewa jukumu la kusimamia usalama na ubora wa bidhaa za chakula kupitia Sheria Na. 2 ya Viwango Sura ya 130. Shirika linatekeleza jukumu hili kupitia kanuni ya usajili na udhibiti wa shehena ya mwaka 2021.

Licha ya elimu kubwa inayotolewa juu ya taratibu bora za uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za chakula, Shirika limebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao bado wanakiuka taratibu zilizowekwa hasa kwenye vinywaji laini (carbonated soft drinks) kwa kuingiza bidhaa zenye mchanganyiko wa sukari na vikoleza utamu (artificial sweeteners) kinyume na matakwa ya viwango vilivyowekwa.

Kwa taarifa zaidi, fungua linki ifuatayo;

taarifa kwa umma kuhusu matumizi ya mchanganyiko wa sukari na vikoleza utamu (artificial sweeteners) kwenye vinywaji laini vyenye kaboni (cardonated soft drink)