Announcements

Posted On: Feb 03, 2023


UFAFANUZI KUHUSU USALAMA WA KINYWAJI CHA JUISI YA EMBE YA AZAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kutoa ufafanuzi wa kitaalam juu ya taarifa inayosambaa
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu bidhaa ya juisi ya embe ya Azam inayozalishwa na kiwanda cha
Bakhresa Food Products Limited kuwa na kiambato kiitwacho “Sodium benzoate (E211)” ambacho
kimedaiwa kuwa si salama kwa afya ya watumiaji.

Kwa maelezo zaidi tafadhali fungua kiambatanisho kifuatacho;

tangazo kuhusiana na usalama wa juisi ya azam